Pages

Saturday, June 6, 2015

BAADA YA KUSITISHA MKATABA NA CANDY N CANDY YA NCHINI KENYA "TOP C" MPYA HII HAPA.

By Eva godchance


Heatmaker wa "Sababu ya Ulofa" Top C ameelezea sababu za kujiondoka katika label ya Candy n Candy ya Nchini Kenya
ni Pamoja na mmiliki wa label hiyo kukiuka masharti ya mkataba  kama vile kurecord nyimbo bila usambazaji mzuri kwenye vyombo vya habari, pamoja na mipango ya mizuri ya matamasha , ni moja kati ya vitu vilivyochangia yeye kuendelea kuwa kimya kwa mda mrefu. Nyota huyo wa Bongofleva kwa sasa amekuja na wimbo mpya unaoitwa "Niamini" ulitengenezwa na producer Ally Zee chini ya studio za Spear Kick record iliyoko nchini Kenya. Top c amesema hayo Akiwa anahojiwa na Nemmykim kupitia Arusha One Radio, pia Top C kwa sasa ni baba mwenye familia ya watoto watatu , na Kwa sasa Hayupo  chini ya Record label yoyote kwani anafanya kazi  zake na kuzisimamia mwenyewe. Pia Top c amewaomba  mashabiki wake wampokee na kumsapoti kwa huo wimbo wake mpya "Niamin"

No comments:

Post a Comment