By Eva godchance
Rapa wa kike anayechipukia kwenye mziki wa bongofleva Hd kutokea Arusha Ni moja kati ya wasanii ambao wanandoto ya kuziba mapengo ya rapa wakike waliokuja na kupotea.
Na Moja kati ya wasanii waliofanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya kwa upande wa wadada ni pamoja na Sister P , Chiku K, Rapii na Witness na kwa sasa nafasi zao huenda zikachukuliwa na rapa wanaochipukia kwa kasi kma HD, Kemiko na Stoshi, ambapo mwanadada HD ameeleza kuwa yeye anayouwezo wa kurap na kuimba pia Hd ameelezea moja kati ya sababu zinazomkwamisha yeye na kushindwa kufanya vizuri katika muziki wa bongofleva ni pamoja na kukosa sapoti kubwa ya mashabiki na management nzuri ya kusimamia na kusambaza kazi zake . Rapa huyo kutoka kaskazini mwa Tanzania Hd ameshafanya nyimbo mbalimbali kama "Kazi ni kazi" aliyomshirikisha PNC pia "Kukupenda" aliyomshirikisha Hush B aliyoifanya Noiz Mekah production chini ya producer mkongwe kutoka Arusha Defxtro Dx. Studio nyingine aliyowahi kufanya nayo kazi ni pamoja na Kiumbe Record iliyoko Dar es Salaam wimbo unaoitwa "Mabishoo" aliyomshirikisha "Baba Byser" .Rapa Hd moja kati wasanii ambao anatamani kufanya nao Collabo ni pamoja na Linex, Diamond, Jay D na Barnaba Boy.
No comments:
Post a Comment