By Nemmy Kim.
Mwisho wa wiki iliyopita Bobbi Kristina ambaye ni mtoto pekee wa marehemu mwanamuziki wa Marekani Whitney Houston alianguka bafuni na kukimbizwa hospitali huku hali yake ikielezwa kuwa ni mbaya na kupelekwa Hospitali kwenye chumba cha uangalizi maalumu, ICU.
Imeelezwa kuwa hadi sasa hali yake bado ni mbaya na madaktari wanaomuuguza katika hospitali ya Emory University wamepoteza matumaini na sasa wanaiachia familia yake hatma ya maisha yake.
Chanzo cha habari karibu na familia hiyo kimedai kuwa hatma ya mtoto huyo iko mikononi mwa familia yake ambayo itatoa uamuzi kama atolewe mashine zinazomsaidia kupumua au la, japo msemaji wa familia amekanusha kwamba hakuna ukweli kwenye uvumi huo.
Baba yake Bobbi ambaye ni Bobby Brown ana imani mtoto wake atapona kwa kuwa katika familia yao kuliwahi kuwa na mgonjwa ambaye alikuwa na hali mbaya kwa muda wa siku nane lakini alipona.
No comments:
Post a Comment