Pages

Sunday, July 19, 2015

MTVMAMA: Diamond ashinda Best Live Act, Wanaijeria wazitawala

By eva godchance

Diamond Platnumz ndio mtumbuizaji bora barani
Afrika.
Hitmaker huyo wa Nana jana alishinda
tuzo ya Best Live Act kwenye MTV MAMA
Awards zilizotolewa jijini Durban, Afrika Kusini


Muimbaji huyo ambaye pia alidondosha show ya
kukata na shoka kwenye tuzo hizo akiwa nabaada ya kuchukua tuzowenye tuzo hizo akiwa na
msanii wa Nigeria, Flavour na kuimba hit yao,
Nana, amewashukuru watanzania na wengine
waliomwezesha kushinda tuzo hiyo.
“Shukran Kubwa sana Zimfikie Mwenyez Mungu
kwa Tuzo hii, na pia Shukran za Dhati Ziwafikie
Wadau, Media, Wasanii na Mashabiki zangu wote
#TeamWasafi kwa kunipigia kura na
Kuhamasisha kwa Nguvu,” ameandika kwenye
Instagram.
“Niushkuru sana Uongozi wangu, Familia pamoja
na Team nzima ya @wcb_wasafi hususan
Madancers wangu kwani Naamini wao ndio
wamenipika nikapikika hadi leo hii kuweza
kuletaTunzo hii Nzito ya Mtumbwizaji Bora
Africa, Nyumbani…lakini pia Shukrani za kipekee
zimfikie Mama yangu kipenzi Sandra kwa
Mafunzo na Malezi anayonipa kila siku juu ya
Dunia,” ameongeza.
“Na Shukran tena za kipekee na aina yake
zimfikie Roho yangu, Kipenzi Changu
@zarithebosslady Kwa raha na Usingizi mwanana
anipatiao na kunifanya nizidi kutunga na kuwa
M’bunifu kwenye kazi..

 #BestLiveAct
#Mtvmama2015 Asanteni sana.”
Hata hivyo ni wasanii wa Nigeria ndio
waliotawala tuzo hizo huku P-Square wakiondoka
na tuzo mbili.

Hii ni orodha nzima
Best Female: Yemi Alade (Nigeria)
Best Male: Davido (Nigeria)
Best Group: P-Square (Nigeria)
Best New Act Transformed by Absolut:
Patoranking (Nigeria)
Best Hip Hop: Cassper Nyovest (South Africa)
Best Collaboration : AKA, Burna Boy, Da LES &
JR: “All Eyes On Me” (SA/Nigeria)
Song of the Year: Mavins: “Dorobucci” (Nigeria)
Best Live: Diamond Platnumz (Tanzania)
Video of the Year: “Nafukwa” – Riky Rick;
Director: Adriaan Louw Best Pop & Alternative:
Jeremy Loops (South Africa)
Best Francophone: DJ Arafat (Ivory Coast)
Best Lusophone: Ary (Angola)
Personality of the Year: Trevor Noah (South
Africa) MAMA Evolution: D’Banj (Nigeria)
Best International: Nicki Minaj Artist of the
Decade: P-Square MTV Base Leadership Award:
Saran Kaba Jones & S’Bu Mavundla.

No comments:

Post a Comment