Uwanjani wanariadha wa Kenya wamekuwa wakililetea taifa hilo medali, lakini unafahamu kuwa wanariadha hao hutumia mda wao mwingine kulihudumia taifa la Kenya?
Kikosi cha Kenya kitakachoshiriki rio, kitawajumuisha wanariadha, ambao mbali na uanamichezo, ni watumishi wa umma nchini Kenya.
Wanariadha, David Rudisha, Jemima Sumgong, Julius Yego na Ezekiel Kemboi, ni miongoni mwa wawakilishi wa Kenya rio watakaovaa sare za wanariadha mbali na sare za askari.
Rais Uhuru Kenyatta, akiikabidhi timu ya Kenya ya olimpiki bendera, aliwashangaza wengi alipotoa wito kwa Ezekiel Kemboi na kumuita 'mlinzi wangu, na wengi walishangaa kwani hawakufahamu alikuwa mlinzi wa Rais.
'Huyu ni askari wangu, Bwana Kemboi,'' Nawatakia kila la heri. alisema.
Miongoni mwa maafisa wa Polisi watakaoiwakilisha Kenya ni David Rudisha, Ezekiel Kemboi, Asbel Kiprop, Geoffrey Kamworor, bingwa mbio za mita elfu kumi, 10000m, Vivian Cheruiyot, na Eunice Sum. Hali kadhalika, Kenya itawakilishwa kwenye mbio za 3000m kuruka viunzi na maji na afisa wa polisi Hyvin Kiyeng.
No comments:
Post a Comment