Ametangaza azma hiyo Ijumaa hii kwenye msikiti wa Taqwah jijini Dar es Salaam. Amedai kuwa kuanzia sasa atakuwa akimtumikia Mungu zaidi.
Amesema ataongea na waandishi wa habari hivi karibuni kuhusiana na uamuzi wake na hatma ya kundi lake la Jahazi Modern Taarab.
Wimbo wa mwisho alioutoa Mzee Yusuf ulikuwa Hewallah aliomshirikisha Vanessa Mdee.
No comments:
Post a Comment