Pages

Monday, September 12, 2016

INTERTAINMENT; Alikiba kutumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA, Oktoba 22

By Nemmy Kim.

Muimbaji wa Aje, Alikiba ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA huko Johannesburg, Afrika Kusini. 

Kupitia mtandao wa Instagram wa meneja wa msanii huyo, Seven Mosha ameweka picha ya msanii wake huyo na kuandika ujumbe unaosomeka, “The King @officialalikiba is set to perform at the MTVAfrica Music Awards 2016 .”

Pia MTV Base wameandika: Yes,@OfficialAliKiba to bring that HEAT to the stage ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ.”
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome, Jumamosi ya Oktoba 22, mwaka huu. Wasanii wengine wanaotarajia kutumbuiza kwenye tuzo hizo ni pamoja na Yemi Alade, Nasty C, Babes Wodumo na wengine wengi. Kwa mwaka huu tuzo hizo zina vipengele 18 ambavyo wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika watawania.

No comments:

Post a Comment