Pages

Tuesday, October 1, 2019

NEWS;R.KELLY AMESEMA AKUMBWA NA MATATIZO YA KIAFYA AKIWA JELA

By Creator,

Mwanamuziki wa RnB kutoka nchini Marekani afya yake ipo mashakani huku akiwa bado yupo jela huko Chicago.

zimepatikana nyaraka ambazo alikuwa nazo mwanasheria wa R.Kelly, mwanasheria huyo amesema mwimbaji R.Kelly mwenye umri wa miaka 52 anapata matatizo ya kiafya kutokana na kutopata uangalizi wa daktari na pia umri wake anapaswa kuwa karibu na madaktari, hayo aliyasema Steve Greenberg ambaye ni mwanasheria wa R.Kelly.
Mwimbaji huyo haruhusiwi kutembelewa kwa pamoja na wanadada wawili ambao alikuwa akiishi nao chicago nyumba moja  "Trump House"
 kwa mujibu wa TMZ, Mwanasheria Greenberg amesema pale Clary atakapomtembelea R.Kelly basi inabidi ipite zaidi ya siku 90 ndipo anaweza kutembelewa na Joycelyn Savage japo wanadada hao ni marafiki.
 Mwezi September iliripotiwa R.Kelly kupunguziwa baadhi ya masharti aliyokuwa amewekewa.Pia Hakimu wa kesi ya R.Kelly amesema kesi hiyo itasikilizwa tena ifikapo April 27, 2020 Ambapo R.Kelly anakabiliwa kesi ya unyanyasiji wa kijinsia na ngono dhidi ya watoto.

No comments:

Post a Comment