Pages

Friday, January 23, 2015

NEWS: Rihanna ashinda kesi dhidi ya Topshop

By Nemmy Kim.


 Rihanna ameshinda kesi ya madai dhidi ya duka la mavazi la Topshop juu ya fulana iliyobandikwa sura yake.
Duka hilo liko mtaa wa maduka yenye mavazi ghali nalo limekata rufaa kutokana na maamuzi ya kuwa kuuza fulana zenye picha hiyo bila makubaliano na mhusika ni kosa la jinai na hakuna haki miliki iliyowekwa dhidi ya bidhaa hiyo.
Lakini katika kile kinachoonekana kama maamuzi muhimu ilibidi yachukuliwe kuzuia uuzwaji wa fulana hizo za kata mkono.
Wakili wa mwanamuziki huyo nguli wa miondoko ya POP anadai kwamba picha inayoonekana katika fulana hiyo haikuruhusiwa kutoka,na ilichukuliwa wakati nyota huyo alikuwa akichukua picha za video huko Kaskazini mwa Ireland kwa ajili ya wimbo wake ulioachiliwa mwaka 2011,na hivyo duka hilo la Topshop linabaki na zuio hilo la kutokuwa na haki ya kuuza bidhaa hiyo.
Duka hilo kubwa lilijitetea kuwa limekuwa likichapisha sura za wasanii miaka kadhaa iliyopita katika fulana na Rihanna si wa kwanza,wapo waliotangulia kama Elvis Presley, Jimi Hendrix na Prince.
Kutokana na hali hiyo Geoffrey Hobbs wakili anayetetea duka hilo anadai kuwa kuwazuia kutouza bidhaa hiyo ni matumizi mabaya ya sheria .
Bwana Hobbs ameongeza kwamba jamii haiamini kwamba kila sura ya mtu maarufu unayoiona katika vazi basi imepewa ruhusa na mhusika,hata hivyo Rihanna ameshafanya biashara na kupata faida kubwa na maduka makubwa ya mavazi kama Topshop wenyewe na mpinzani wake River Island.
Hakuishia hapo katika kukosoa hukumu hiyo ya maahakama kuu kwamba watu maarufu hawana mamlaka ya kuingilia kazi zao za uzalishaji na Topshop walipoamua kutumia sura ya mwanamuziki huyo haina maana kuwa wamempitia tu lah.
Hukumu hiyo inadaiwa ilikuwa imeangazia na kulinda hadhi na heshima ya msanii huyo asije akaharibiwa nia yake njema katika tasnia ya mavazi.

No comments:

Post a Comment