Pages

Wednesday, August 12, 2015

Tanzania inatumia sera ya utamaduni ya mwaka 1997, BASATA yawataka wasanii wapiganie wapate sera mpya

By eva godchance 

Tanzania bado inatumia sera ya utamaduni ya
taifa ya mwaka 1997.

Hiyo ni tofauti kidogo na
Kenya ambayo imezindua sera ya muziki ya taifa
leo.
Taarifa hiyo imetolewa na baraza la sanaa la
taifa, BASATA baada ya muimbaji na mtunzi wa
nyimbo, Lameck Ditto kulitaka baraza hilo liige
mfano wa Kenya.
“Lengo la kuwa na sera ya Sanaa lipo.Kwa sasa
sera ya utamaduni ya mwaka 1997 ndiyo
inatumika.Wasanii tulisukume hili,” BASATA
limesema kwenye Twitter.
Hata hivyo BASATA limesema wizara
inayosimamia sanaa ya Kenya ni tofauti na ya
Tanzania ambayo ina mambo mengi ndani yake
na muziki upo chini ya idara ya utamaduni.
“Kwa Kenya Sanaa ni Idara chini ya Wizara kwa
hapa kwetu Sanaa ni kitengo chini ya Idara ya
Utamaduni. Kenya inaitwa Wizara ya
Michezo,Utamaduni & Sanaa,kwetu ni
Habari,Vijana,Utamaduni & Michezo.Kuna tofauti
kubwa,” limesisitiza.

No comments:

Post a Comment