Belle 9 Akizungumza na waandishi wa habari.
Mastaa wa muziki, filamu pamoja na viongozi wa serikali Jumamosi hii walipamba usiku wa uzinduzi wa video mpya ya Belle 9 ‘Give IT TO ME’.
Tafrija hiyo fupi ambayo iliandaliwa na kampuni ya muimbaji huyo,Vitamin Music Group Limited, iliwakutanisha wadau mbalimbali wa muziki pamoja na waandishi wa habari.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ni mmoja kati ya viongozi wajuu waliohudhuria uzinduzi huo.
Akiongea katika uzinduzi huo, Belle aliishukuru team nzima ya Vitamin Music Group Limited kwa kufanikisha tukio hilo pamoja na wadau mbalimbali ambao walijitokeza usiku huyo kwa ajili ya kumsupport. Angalia picha.
Itazame video ya Belle9 ft G-warawara_"Give it to Me" 👇👇👇
No comments:
Post a Comment