Pages

Wednesday, August 10, 2016

NEWS; Linex aeleza kinachokwamisha kufanyika kwa video ya wimbo ‘Hewala’ alioshirikiana na Bella

By Nemmy Kim.

Msanii wa muziki Linex Sunday Mjeda amefunguka kwa kusema kuwa wimbo ‘Hewala’ haujafanya vizuri zaidi kutokana na kuchelewa kwa video ya wimbo huo.

Linex amesema hali hiyo imeathiri rotation ya wimbo huo kutokana na mashabiki kuzoea mtindo wa kutoa audio na video kwa pamoja.
“Ngoma imeenda kwa kiasi chake na kama tungetoa na video ingeenda zaidi,” alisema Linex “Mashabiki wengi wameanza kuuzoea mtindo wa kutoa audio pamoja na video. Lakini yote yamesababishwa sisi kuwa busy, Bella amekuwa na tour za hapa na pale, mimi nadhani pia, lakini mambo yanaweza kukaa sawa hivi karibuni na video tukashoot, tunamshukuru Mungu ngoma inaenda poa”
Pia Linex amewataka mashabiki wake kuendelea kuusupport wimbo huo kwa kuwa kuna mambo mazuri yanakuja.

No comments:

Post a Comment